Klose avunja rekodi ya ufungaji mabao

Klose ndiye mfungaji mabao mengi zaidi ya kombe la dunia 16.
Maelezo ya picha,

Klose ndiye mfungaji mabao mengi zaidi ya kombe la dunia 16.

Mshambulizi wa Ujerumani Miroslav Klose ameweka rekodi ya kuwa mfungaji mabao mengi zadi katika historia ya kombe la dunia.

Klose alifunga bao la pili Ujerumani ilipoisakama Brazil mabao 7-1 katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya kombe la dunia huko BELO HORIZONTE,Brazil.

Klose mwenye umri wa miaka 36 amefunga sasa jumla ya mabao 16 baada ya kushiriki michuano nne za kombe la dunia.

Mshambulizi huyo alikuwa ametoshana na mshikilizi wa zamanai wa rekodi hiyo mbrazil Ronaldo alipoifungia Ujerumani bao la pili la kusawazishia dhidi ya Ghana katika mechi za mchujo awali katika kipute hicho.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Klose amefunga mabao 16

Wakati huohuo mshambulizi huyo alivunjilia mbali rekodi ya mfungaji mabao mengi zaidi ya kimataifa kwa mjerumani alipoifungia timu yake bao la 68 Ujerumani ilipokuwa ikishiriki mechi ya kirafiki dhidi ya Armenia.

Rekodi ya awali ya Ujerumani ilikuwa inashikiliwa na Gerd Mueller

Kufuatia Ushindi huo Ujerumani imefuzu kwa fainali yake ya kwanza katika kipindi cha miaka kumi na miwili iliyopita.