Bingwa wa Tour de France Froome ajiondoa

Image caption Bingwa wa Tour de France Chris Froome amejiondoa mbioni baada ya kuanguka mara mbili.

Bingwa wa Tour De France mzaliwa wa Kenya Chris Froome amejiondoa kutoka mashindano ya mwaka huu baada ya kuanguka mara mbili katika mkondo wa tano.

Froome alijiondoa baada ya kutegwa na kuanguka zikiwa zimesalia kilomita 66 mkondo wa tano kukamilika.

Mwendesha baiskeli huyo mtajika alilazimika kupanda gari la dharura la kundi la Team Sky alipozidiwa na uchungu

Froome aliwambia mashabiki wake kupitia mtandao wa kijamii wa tweeter 'Kuwa anajuta kujiondoa baada ya uchungu kwenye mkono wake kuzidi na kufanya kumiliki usukani kuwa ngumu.''

Image caption Bingwa wa Tour de France Chris Froome amejiondoa mbioni baada ya kuanguka mara mbili.

''Nitarejea nyumbani hii leo ilinipate matibabu kikamilifu kwa sababu ya majeraha ya mkono.''

Froome alijiondoa akiwa katika nafasuii ya saba sekunde mbili pekee yake nyuma ya kinara wa mbio hizo Vincenzo Nibali.

Hapo jana alikuwa ameruhusiwa kurejelea mashindano baada ya kunguwaa na kujeruhi kiuno lakini picha za X-Ray zilionesha kuwa hakuwa na majeraha yeyote.