Ni Argentina dhidi ya Ujerumani Fainali

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kipa wa Argentina Sergio Romero alikuwa Nyota wa mechi hiyo

Argentina imejukatia tikiti ya kufuzu kwa fainali yake ya kwanza tangu mwaka wa 1990 ambapo itachuana Ujerumani.

Argentina ilikuwa imetoka sare tasa baada ya muda wa kawaida na ule wa Ziada na hivyo kulazimu mechi hiyo kuamulia kwa mikwaju ya penalti.

Kipa wa Argentina Sergio Romero ndiye aliyekuwa nyota katika mechi hiyo baada ya kuokoa mikwaju miwili na kuipa Argentina Ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Uholanzi.

Image caption Kipa wa Argentina Sergio Romero alikuwa Nyota wa mechi hiyo

Romero aliokoa mikwaju ya Ron Vlaar na Wesley Sneijder.

Wafungaji wa Argentina walikuwa ni Lionel Messi,Ezequiel Garay Sergio Aguero na kisha Maxi Rodriguez.

Argentina sasa Itachuana na Ujerumani ambayo iliweka historia kwa kuinyuka Brazil mabao 7-1katika nusu fanali.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kocha wa Argentina Alejandro Sabella amefurahia kufuzu kwa fainali.

Uholanzi ambayo sasa imeshindwa kutwaa kombe la dunia hata baada ya kufuzu kwa nusu fainali tatu mfululizo itachuana dhidi ya wenyeji Brazil siku ya jumamosi kuamua mshindi wa tatu.

Brazil ilipata kipigo cha mabao 7-1 dhidi ya Ujerumani siku ya Jumanne.

Penalti ndizo zitakazoamua nani kati ya Uholanzi na Argentina atakutana na Ujerumani katika fainali.

00:45 Mpira umekwisha .Sasa ni dakika 30 za muda wa ziada.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Argentina 0-0 Uholanzi 85''

00:43 Hakuna mechi ya Nusu fainali ya kombe la dunia ambayo imeishia sare tasa hata baada ya muda wa ziada.

00:42 Argentina 0-0 Uholanzi 82''

00:40 Argentina wanafanya mabadiliko ya wachezaji wawili kwa mpigo.

00:06 Demichelis anaoneshwa kadi ya Njano baada ya kumwangusha Arjen Robben

00:05Uholanzi 0-0 Argentina 45'' Kipindi cha pili kimeanza .

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mshambulizi wa Argentina Messi amezimwa

23:45+2Kipindi cha kwanza kimekamilika .

23:45 +1 Kufikia wakati kama huu hapo jana Ujerumani ilikuwa imemfunga Brazil mabao 5-0

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mashabiki katika uwanja wa sao Paolo

23:45 Uholanzi 0-0 Argentina 45''

23:44 Martins Ndi (uholanzi) aoneshwa kadi ya kwanza ya manjano

23:23 Kona nyengine kuelkea upande wa Uholanzi ,duh unatoka nje na inakuwa ni Goalkick

23:20 Kona ya kwanza kuelekea upande wa Uholanzi,,,lakini Wapi inazimwa

23:20 Argentina 0 -0 Uholanzi

23:14 Messi ndiye anaupiga lakini kipa Cillessen wa Uholanzi anaudaka bila wasiwasi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Sao Paolo Argentina vs Uholanzi

23:13 Perez anaopatia Argentina Freekick ya pili nje tu ya eneo

23:10 Argentina 0-0 Uholanzi

23:09 Messi anapata FREEKICK ya kwanza kuelkea kwa Argentina

23:00 Mpira unaanza hapa sao Polo Argentina dhidi ya Uholanzi .

22:59 Perez amechukua nafasi iliyowachwa na Di Maria upande wa Argentina

22:59 Van Persiena De Jong wanaanza kwa upande wa Uholanzi

22:57 Wimbo wa taifa unachezwa hapa Sao Paolo

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Shabiki wa Uholanzi

22:55

22:54Wachezaji wa Argentina Sergio Aguero na Marcos Rojo wamerejea

22:54 Mshambulizi wa Bracelona Lionell Messi atakabidhiwa majukumu mahsusi ya kuifikisha Argentina katika fainali yao ya kwanza tangu mwaka wa 1990.

22:53 Argentina wanatatizika kwa kumkosa mchezaji wa kutegemewa Angel Di Maria ambaye amejeruhi paja

22:52 Uholanzi tofauti na Argentina imefuzu kwa fainali ya kombe la dunia mara mbili zilizopita ikimaliza ya pili mara mbili mfululizo .

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mashabiki wa Argentina wakisubiri mechi hiyo ya kihistoria

22:51 Argentina inatafuta tiketi yake ya kwanza ya Fainali tangu mwaka wa 1990

22:50 Argentina inachuana na Uholanzi katika mechi ya pili ya nusu fainali ya kombe la dunia Brazil