Scolari kuamua hatma yake baada ya kombe

Haki miliki ya picha
Image caption Scolari kuamua hatma yake baada ya kombe la dunia

Kocha wa Brazil Luiz Felipe Scolari amesema kuwa ataamua mustakabal wake baada ya kombe la dunia.

Scoalari aliyasema hayo baada ya aibu ya kutandikwa mabao 7-1 na Ujerumani katika mechi ya kwanza ya nusu fainali Jumanne.

Vyombo vya habari vilimlimbikizia lawama kwa kichapo hicho lakini Scolari amesema kuwa atatua kauli yake baada ya mechi ya kuamua mshindi wa tatu dhidi ya Uholanzi siku ya Jumamosi.

Kichapo hicho ndicho kilikuwa kibaya zaidi kuwahi kuipata Selecao tangu mwaka wa 1920 Brazil ilipolimwa 6-0 na Uruguay.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Scolari kuamua hatma yake baada ya kombe la dunia

Kocha huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 65 alikuwa ameiongoza Brazil mwaka wa 2002 lakini akondoka na kurejea mwaka wa 2012 kuiandaa timu hiyo kwa mashindano haya ya nyumbani.

Brazil walikuwa nyuma mabao 5-0 baada dakika 30 ya kipindi cha kwanza kabla ya kukamilisha mechi hiyo mabao 7-1.