Rudisha aweka mda bora mwaka huu

Haki miliki ya picha PA
Image caption David Rudisha

Bingwa wa michezo ya Olimpiki katika mbio za mita 800 duniani David Rudisha amesawazisha rekodi ya muda bora zaidi duniani mwaka huu baada ya kushinda mbio za mita mia nane katika mbio za Almasi mjini Glasgow siku ya jumamosi.

Rudisha ambaye bado anaendelea kupona jereha la goti lililomzuia kushirki katika riadha msimu wote wa mwaka 2013,alirudi kwa kishindo nchini Uingereza kwa mara ya kwanza tangu kuvunja rekodi katika michezo ya Olimpiki mjini London na kushinda mbio hizo za jumamosi kwa dakika moja sekundi 43.34.

Mkenya huyo alimshindi mpinzani wake wa karibu kutoka Afrika kusini Andre Olivier kwa zaidi ya mita hamsini na kusawazisha rekodi hiyo iliowekwa na mkenya mwengine Asbel Kiprop wiki iliopita.

Hatahivyo alishidwa kuipiku rekodi yake ya dakika moja sekunde 40 aliyoweka wakati wa mashindano ya Olimpiki mjini London mwaka 2012.