Huwezi kusikiliza tena

Vijana wa Kenya warejea kutoka Brazil

Timu ya vijana walio chini ya umri wa miaka 18 ya Trans Nzoia Youth Sports Association, kwa kifupi TYSA, kutoka nchini Kenya wamerejea nyumbani baada ya kushiriki kwenye mashindano ya wachezaji watano kila upande ya Football For Hope Festival mjini Rio De Janeiro, Brazil.

Timu ya Delta Culture ya Cape Verde ilishinda mashindano hayo kwa kuilaza Sport Dans La Ville ya Ufaransa bao 1-0 mechi ya fainali.

Timu hiyo ya Cape Verde na Tysa ni baadhi ya timu nane za Afrika zilizoshiriki mashindano hayo yaliyojumuisha timu kutoka mataifa 32.

TYSA ilimaliza mechi zake zote bila kupoteza.

Wachezaji hao, ambao walitizama mechi ya robo-fainali kati ya Ujerumani na Ufaransa wanasema mbali na kandanda, wamejifunza mengi kuhusu maadili na jinsi ya kupambana na maisha kwa jumla.

John Nene amezungumza nao mjini Nairobi akianza na nahodha George Waweru kwa jina la utani Beckham ambaye ni miongoni mwa wachezaji wanne wa TYSA waliosafiri kwa ndege kwa mara ya kwanza na wanatueleza mengi kuhusu walivyojihisi kuwa angani kwa mara ya kwanza.