Diego Costa ajiunga na Chelsea

Haki miliki ya picha Getty

Mshambulizi wa Atletico Madrid,Diego Costa hatimaye amejiunga na klabu ya Chelsea kwa miaka mitano ijayo.

Kijana huyo raia wa uhispania yasemekana amelipwa £32m

''Nafurahi kujiunga na Chelsea kwani kila mtu anaitambua kutokana na ushindani wake,'' Costa alisema huku akieleza furaha yake ya kujiunga na ulaya.

Costa amekuwa mchezaji wa tatu kujiunga na Chelsea baada ya Cesc Fabregas na Mario Pasalic.

Mshambulizi huyu amefungia Atletico mabao hamsini na mbili msimu uliopita ambapo walishinda taji la kwanza la LaLiga tangu 1996 na kufikia kuwa mabingwa wa ligi.

Kocha wa chelsea Jose Mourinho aliongeza mshambulizi matata katika kipindi hicho.

Klabu hii ya ulaya ilifunga mabao sabini na moja kwenye ligi msimu uliopita chini na mabao thelathini na moja dhidi ya mabingwa Manchester city waliomaliza kwa pointi nne mbele yao.

Fernando Torress,Demba na Samuel Etoo walipambana kushikilia nafasi zao.

Costa atajiunga na mchezaji mwenza wa kimataifa Sesc Fabregas kutokana na matokeo duni ya uhispania katika kombe la dunia ambapo walibanduliwa nje katika hatua ya kwanza ya kikundi.