Pesa si msukumo ulionileta QPR-Ferdinand

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rio Ferdinand ni mmoja wa wachezaji wakongwe waliokuwa wakichezea Man United

'Nimepata mikataba chungu nzima, lakini kwangu msuko si pesa? Hayo maneno yake Rio Ferdinand,

akizungumzia kutia kwake saini mkataba na klabu ya QPR.

Kama si hela basi kipi kimempa raha hiyo mlinzi huyo wa zamani wa Man Utd na kikosi cha Unigereza?

Amesisitiza kusema-'Offa hizo kemkem zilimiminika kutoka kote ulimwenguni tena nyengine za mapesa mengi lakini mimi raha yangu ni kucheza katika Premier League, nahisi nnakipaji kitakachosaidia kuiweka klabu hii katika nafasi nzuri katika ngazi ya Premier League."

Basi kama kweli kwa Ferdinand hela si hoja.Katika soka kama vile katika maswala mengine mengi hela ni hoja. Na kutathmini kujua je msimu huu nani ana pochi zito na atalifungua kwa kisiasi gani na kwa manfaa gani mambo ni kama hivi.

Liverpool tayari imevuna £75m kutoka Barcelona alikohamia mchezaji wao Suarez. Lakini je wataipiku Tottenham ambao msimu uliopita ilipata £80m kwa fidia ya uhamiaji wa mchezaji wao wa mwaka Gareth Bale alipokwenda Real?

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Je Drogba atahamia tena Chelsea?

Wengineo kama hao hao Spurs waligharamika si haba kwa kuleta wachezaji wengine lakini wakaishia kumaliza nje ya nne bora.

Je ndio sababu Msimu huu haiajatoa hata peni kusajili mchezaji mpya?

Nao vigogo mwenye pochi kubwa Man Unitedna na kocha wao mpya Van Gaal wanasubiriwa ikiwa wataongeza vinara wengine wa soka baada ya kuwatwaa Luke Shaw na Herrera.

Arsenal nao vipi? Tayari Wenger ameshatoa £35m kwa Alexis Sanchez atoke Barcelona na bado kuna wachezaji kama wanne hivi wanaowamezea mate.

Na je eti Jose Mourinho anawaza kumrudisha Didier Drogba Chelsea kunakoonekana kuwa na upungufu wa washambuliaji? Huku tayari akiwa kesha mpata Diego Costa , Cesc Fabregas na Luis Felipe.

Mabingwa Man City hawajaachwa nyuma , lakini je....watafanikiwa kumshawishi Yaya Toure abaki nao baada ya Toure kitishia kuondoka kutokana na sintofahamu ya mwezi uliopita? .