Tanzania sare 2 - 2 na Msumbiji

Image caption Timu ya taifa ya Tanzania "Taifa Stars"

Tanzania ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani Taifa Stars imeshindwa kutamba mbele ya majirani zao kutoka kusini Msumbiji baada ya kulazimishwa sare ya bao 2 - 2 katika kuania kucheza michuano kombe la Mataifa ya Afrika.

Wakati Tanzania ikitoka sare na Msumbiji majirani zao Kenya wakiwa Huko Lesotho, wameshindwa kutamba na hivyo wakaambulia kupigwa bao 1 - 0.

Nchi ya Afrika mashariki iliyofurukuta ni Uganda iliyokwamisha 2 - 0 dhidi ya Mauritania. Huko Benin, Malawi imepigwa bao 1 - 0

Bila shaka Wacongo wamekesha wakicheza muziki baada ya kuwavumishia majirani zao Rwanda kwa bao 2 - 0

Sierra Leone nao wakawabamiza ushelisheli bao 2 - 0.