Mourinho : Drogba ni Chelsea damu.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mourinho : Drogba ni mChelsea damu.

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amesema kuwa Mshambulizi wa galatasaray ya Uturuki Didier Drogba ni Mchelsea damu .

Mshambulizi huyo wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 36 aliwahi kushinda mataji 10 akiwa stamford Bridge kuanzia mwaka wa 2004-2012 kabla ya kuguria Galatasaray.

Mourinho alidhibitisha kuwa The Blues inatafakari kurejea kwake Uingereza na kuwa anatumai uhamisho huo utatekelezwa bila hisia kali .

"Nikifaulu kumrejesha Uingereza jambo ambalo natumai litafanyika kwa haraka ,itakuwa kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa kuimarisha kikosi na timu kwa jumla''.

Drogba, alijiunga na Chelsea mwaka wa 2004 akitokea Marseille katika uhamisho ulioigharimu klabu hiyo pauni milioni £24.

Wakati huo aliiongoza Chelsea kutwaa mataji matatu ya ligi kuu ya Uingereza mataji 4 ya FA , mataji mawili madogo ya ligi mbali na ubingwa wa bara Ulaya .

Haki miliki ya picha c
Image caption Drogba akiwa Galatasaray.

Aliondoka Stamford Bridge mwaka wa 2012 baada ya kutinga penalti iliyoisaidia klabu hiyo kutwaa kombe la mabingwa barani Ulaya dhidi ya Bayern Munich .

Drogba aliwahi kuichezea klabu ya China Shanghai Shenhua, kabla ya kuijunga na Galatasaray January 2013.