Jason Dunford atangaza kustaafu

Image caption Jason Dunford akiwa mjini Glascow

Aliyekuwa bingwa wa Jumuiya ya madola katika shindano la uogeleaji mita 50 Butterfly, Mkenya Jason Dunford ametangaza kuwa atastaafu rasmi baada ya mashindano ya mwaka huu.

Akiongea baada ya kuondolewa kwenye shindano hilo baada ya kumaliza katika nafasi ya tano, Dunford amesema kuwa, ameamua kuchukua uamuzi huo kutokana na kile alichokitaja kama ukosefu wa msaada wa kutosha kutoka kwa wasimamizi wa michezo nchini Kenya.

Amelalamika kuwa hakupewa vifaa vya michezo ili kumwezesha kushiriki vyema katika mashindano ya mwaka huu.

Amesema, kinyume na mashindano mengine alipata mavazi yake ya michezo siku moja tu kabla ya kuingia kidibwini.