Wanariadha wa Kenya walalama Scotland.

Image caption Wanariadha wa Kenya wakiwa mjini Glascow

Kikosi cha Kenya katika mashindao ya Jumuiya ya madola, yanayoendelea mjini Glascow, kinakabiliwa na wakati mgumu, kutoka na matatizo kadhaa.

Sasa imebainika kuwa baadhi ya wanariadha wa Kenya hawana vifaa vya michezo.

Naibu kiongozi wa ujumbe wa Kenya Tecla Lorupe amesema kuwa wao walifahamishwa siku ya Alhamisi kuwa baada ya wanariadha hawajapokea vifaa na sare zao za michezo.

Lorupe ambaye, ni bingwa wa zamani wa dunia katika mbio za masafa marefu za Marathon, amesema wao wameshangazwa sana na tukio hilo.

Image caption Wanariadha wa Kenya katika mashindano ya Jumuiya ya Madola mjini New Delhi

Amesema kumekuwa na matatizo ya kuwasilisha vifaa hivyo vya wanamichezo wa Kenya, kutoka kwa kampuni inayotengeneza mavazi hayo.

Aidha amesema nusura mabondi wa Kenya wakose kushiriki katika mashindano ya mwaka huu, kutokana na ukosefu wa vifaa vyao.

Lorupe amesema walipata bahati wakati, kamishna wa michezo nchini Kenya Gordon Oluoch alipolazimika kutumia fedha fedha zake kununua vifaa hivyo ambavyo vilitumika na mabondia siku ya Ijumaa.

Siku ya Alhamisi, muogeleaji wa Kenya Jason Dunford aliondolewa katika shindano ya mita hamsini butterfly, kutokana na kile alichokitaja kama kutopata vifaa kwa wakati unaofaa.

Mbali na wanariadha kukosa vifaa na mavazi yao, wasimamizi wa michezo mbali mbali nao wanalalamika kuwa hawajapata marupurupu yao.

Hali hii imelleta wasi wasi katika kambi ya kenya huku baadhi ya wanariadha wakiondolewa mapema katika mashindano ya mwaka huu.

Image caption Tecla Lorupe

Baadhi yao wanasema, hali duni katika kambi ya maandalizi na hapa mjini Scotland huenda ikaadhiri matokeo ya timu ya Kenya.