Arsenal yamsajili Calum Chambers

Haki miliki ya picha ArsenalFC
Image caption Arsenal yamsajili Chambers

Kilabu ya Uingereza ya Arsenal imemsajili mlinzi wa kilabu ya Southampton Calum Chambers kwa takriban paundi millioni 16.

Mchezaji huyo wa timu ya Uingereza isiozidi umri wa miaka 19 alifanyiwa ukaguzi wa kimatibabu siku ya ijumaa.

Chambers mwenye umri wa miaka 19 ameshiriki mara 25 katika timu ya soka ya taifa la Uingereza na kwamba Arsenal inamuona kama suluhu wa safu ya ulinzi wa kulia na katikati .

Arsenal pia inamsaka mchezaji wa kiungo cha kati wa Southampton Morgan Schneiderlin mwenye umri wa miaka 24 ambaye aliichezea timu ya Ufaransa katika kombe la dunia.