FIFA inachunguza ubaguzi wa rangi

Image caption FIFA yaanzisha Uchunguzi kuhusiana na Ubaguzi wa rangi dhidi ya wachezaji wa Manchester City

Fifa imeanzisha uchunguzi kubaini ukweli wa madai ya mchezaji wa Manchester City kuwa alidhulumiwa kutokana na rangi yake timu hiyo ilipokuwa Croatia.

Shirikisho hilo la soka duniani linaendeleza uchunguzi huo kufuatia madai ya Seko Fofana, 20, kuwa alidhihakiwa walipokuwa wakishiriki mechi ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21.

Wakati huohuo shirikisho hilo limeiagiza shirikisho la soka la Italia kuanzisha uchunguzi dhidi ya ,Carlo Tavecchio ambaye anatuhumiwa kwa kutamka maneno ya kuwadunisha wachezaji wenye asili ya Afrika.

Msemaji wa FIFA ameiambia BBC kuwa wanakusudia kutafuta suluhu ya tukio lililompelekea kocha wa City Patrick Vieira kuwaondoa wachezaji wake uwanjani.

Kwa upande wake shirikisho la kandanda la Croatia limeanzisha uchunguzi wake.

Msemaji huyo alisema kuwa mwenyekiti wa jopo la kuchunguza dhulma kwa misingi ya rangi Jeffrey Webb anafuatilia kwa karibu matukio hayo.