Jack Wilshere ajutia uvutaji sigara

Haki miliki ya picha d
Image caption Wishere ajutia kuvuta sigara hadharani

Kiungo wa Arsenal amesema anajutia kitendo chake cha kupigwa picha akivuta sigara hadharani katika bwawa la kuogelea huko Las Vegas.

Wilshere mwenye miaka 22 amelaumiwa hasa kwa kuzingatia wakati picha hizo ziliposambaa timu yake ya Uingereza ilikuwa katika kipindi kigumu ikitolewa katika Kombe la Dunia hatua za mwanzo.

Hii ni mara ya pili Wilshere kufumwa akivuta sigara katika kipindi cha miezi tisa.

Mwezi wa kumi, Wilshere alipigwa picha akivuta sigara akiwa nje ya Klabu ya Usiku baada ya kuishinda Napoli.

"Ninajutia," alisema. "haikubaliki na nitakubaliana na matokeo kisha maisha yataendelea."

Meneja Arsenal, Arsene Wenger alimkosoa Wilshere na akasema ataongea nae kuhusu suala hili.