Divock Origi asajiliwa Liverpool

Haki miliki ya picha Getty

Liverpool imemsajili mshaambuliaji wa Ubelgiji Divock Origi akitokea Klabu yake ya Lile aliyojiunga nayo akiwa na miaka 15.

Mchezaji huyo mwenye miaka 19 ameukubali mkataba huo ameukubali mkataba huo wa miaka mitano lakini ataendelea kubaki kwenye klabu yake huko ufaransa kwa mkopo katika msimu ujao na atahamia Anfield mwaka ujao 2015.

„Ninayo furaha kuona klabu kubwa kama Liverpool ikionyesha kunitaka” Origi alisema.

Origi alicheza mechi zote tano za Ubegiji katika michuano ya kombe la dunia la mwaka huu wakati wakipigana kuelekea robo fainali na kwa mguu wake akaipiga Urusi bao moja.

Klabu ya Liverpool mpaka sasa imemchukua:

Mshambuliaji Rickie Lambert, 32, kwa pauni milioni 4 akitokea Southamptom

Kiungo wa wa kati Adam Lallana, 25, kwa pauni milioni 25 kutoka Southampton

Kinugo Emre Can, 20, kwa pauni milioni 10 akitokea Bayer Leverkusen

Winga Lazar Markovic, 20, kwa pauni milioni 20 akitokea Benfica

Mlinzi Dejan Lovren, 25, kwa pauni milioni 20 akitokea Southamptom

Na sasa Mshambuliaji Divock Origi, 19, kwa pauni milioni 20 akitokea Lile.

“Najua hii ni klab yenye historia nzito, mashabiki na wachezaji wakubwa,” aliongeza.

“Kwangu Liverpoool ni moja ya vilabu bora kabisa duniani na ninayo furaha sana kuwa sehemu ya historia hii.

Origi alianzia katika klabu ya Genk kabla ya kuhamia Lile.