Lampard kulipwa mshahara wake

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Frank Lampard

Manchester City watamlipa Frank Lampard mshahara wake wote wakati akimalizia muda wake kwa miezi sita baada ya kutia saini ya kuhamia New York City hali inayoonyesha huenda ni mbinu ya kukwepa kanuni za matumizi ya fedha zilizowekwa na UEFA.

Lampard mwenye miaka 36 alitia saini mwezi uliopita kwenda kuichezea klabu hiyo ya New York City ambayo kwa kiasi inamilikiwa na mmiliki wa sasa wa Manchester City.

Bosi wa Arsenal, Arsene Wemger ameuliza kama hiyo ni mbinu ya makusudi ya kukwepa kanuni za UEFA zinazotoa muongozo juu ya matumizi ya fedha hasa wakati wa usajili.

Wenger alikuza Sizijui vizuri kanunui sawasawa, lakini walilipia pauni milioni 59.4 ili wacheze marekani msimu ujao.