Refarii mtajika Howard Webb ameestaafu.

Image caption Refarii mtajika Howard Webb ameestaafu.

Refarii mtajika Howard Webb ameestaafu.

Webb ambaye amepuliza kipenga kwa muda wa miaka 25 amestaafu baada ya kuchaguliwa kuwa afisa wa shirikisho la marefarii (Professional Game Match Officials Limited PGMOL).

Kabla ya kustaafu Webb alikuwa muamuzi katika mechi 500 za ligi ya Premia ya Uingereza mbali na zile za kuwania ubingwa wa FA.

Hata hivyo kilele cha tajriba yake ilikuwa fainali ya kombe la dunia la mwaka wa 2010 iliyoandaliwa huko Afrika Kusini .

Refarii huyo mwenye umri wa miaka 43 alianza kazi hiyo mwaka wa 1989.

"najivunia tajriba niliyonayo na sasa nawashukuru wenzangu kwa kunichagua kuwahudumia katika kazi hii mpya ," alisema Webb.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Refarii mtajika Howard Webb ameestaafu.

Webb amewahi kuamua fainali ya kombe la mabingwa barani Ulaya fainali ya ligi kuu ya premia ya Uingereza.

Katika kombe la dunia lililokamilika majuzi huko Brazil, Webb alimua mechi ya kundi Cha baina ya Colombia na Ivory Coast,na ile ya mchujo baina ya Brazil na Chile.

Amewahi tuzwa na malkia wa Uingereza mwaka wa 2011na tuzo la MBE .