Hatimaye Rodriguez apokea tuzo

Image caption Hatimaye James Rodriguez ametuzwa tuzo la mfungaji bora.

Hatimaye mshambulzi wa Colombia James Rodriguez aliyeduwaza ulimwengu kwa kufunga mabao mengi zaidi katika kombe la dunia lililokamilika huko Brazil mwezi uliopita amepokea tuzo lake la mfungaji mabao mengi '' Golden Boot''.

Rodriguez ambaye aliyetikisa wavu mara 6 huko Brazil sasa anakibarua cha kutafuta namba huko Real Madrid dhidi ya wakinzani wenye haiba yake kama mchezaji bora msimu huu Christiano Ronaldo.

Rodriguez alinunuliwa na mabingwa hao wa kombe la mabingwa barani ulaya kutoka Monaco kwa pauni milioni 71.

Mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 23 alisema kuwa anamatumaini makubwa ya kutamba Santiago Bernabéu.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption James Rodriguez akilia baada ya kushindwa na Brazil.

Bao lake dhidi ya Uruguay katika robo fainali ya kombe la dunia limepigiwa upatu kutwaa tuzo la bao la mashindano japo Rodriguez mwenyewe anaikumbuka bao lake la kipekee dhidi ya Japan kuwa bora.

Colombia ilitegemea mabao yake sita katika mechi 5 kufuzu kwa hatua ya robo fainali kabla ya kuambulia kichapo cha 2-1 dhidi ya wenyeji Brazil.