FIFA yaamuru Maigari kurejeshwa Nigeria

Image caption Aminu Maigari amerejeshwa madarakani kufuatia barua ya shirikisho la Soka duniani FIFA.

Aliyekuwa mwenyekiti wa shirikisho la soka la Nigeria Aminu Maigari amerejeshwa madarakani.

Hatua hiyo inafuatia barua ya shirikisho la soka duniani FIFA iliyoiandikia kamati kuu ya shirikisho hilo barua ya kuitaka imejeshe madarakani maramoja.

Kamati kuu ya Shirikisho hilo lilikuwa limepiga kura ya kutokuwa na imani na uongozi wake mwezi mmoja uliopita na hivyo akan'golewa madarakani .

Katika barua hiyo iliyoandikiwa na naibu katibu mkuu wa FIFA Markus Kattner kamati hiyo ilituhumiwa kwa kukiuka vipengee muhimu vya kanuni za FIFA na hivyo ikalazimu Maigari arejee madarakani.

Maigari aliiambia BBC kuwa hakuna mshindi wala aliyeshindwa katika matukio hayo katika shirikisho la NFF .

Image caption Aminu Maigari amerejeshwa madarakani kufuatia barua ya shirikisho la Soka duniani FIFA.

Aliwataka wadau wa kandanda nchini humo waungane kwa manufaa ya maendeleao ya kandanda Nigeria.

takriban mwezi mmoja tu tangu atimuliwe na kamati kuu ya NFF .

Maigari alirejea kwa kishindo katika Afisi za NFF mjini Abuja baada ya Kattner kuamuru kuwa ndiye atakayesimamia uchaguzi mkuu wa kamati kuu ya NFF utakaofanyika tarehe 26 Agosti huko Warri, katika jimbo la Delta.

Isitoshe Fifa imependekeza kuwa uongozi wa NFF urejelee mfumo wake wa kabla ya kombe la dunia la mwaka wa 2014 huko Brazil.

Wadau wa maswala ya kandanda nchini humo hawana matumaini yeyote ya Maigari, aliyechukua NFF Agosti 2010 kurejea uongozini baada ya uchaguzi huo.

Naibu wake Mike Umeh na Chris Giwa ndio wanaogombea kiti cha uenyekiti kwani Maigari hakuruhusiwa kuwasilisha vyeti vya ugombea wa kiti hicho.