Woods ajiondoa katika kombe la Ryder

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Tiger Woods ajiondoa kwenye mashindano ya kombe la Ryder

Mchezaji nyota wa gofu Tiger Wood wa Marekani, amejiondoa katika mashindano ya kombe la Ryder.

Amefanya hivyo baada ya kushauriwa na madaktari wake.

Tiger amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya mgongo mara kadhaa na kufikia usiku wa kuamkia hii leo ameamua kutangaza kujitoa kwenye michuano hiyo ya kimataifa.

Tiger amemuomba kocha wa timu ya Taifa ya Marekani Tom Watson amuwie radhi kwani wataalamu wake wa Afya wamemtaka apumzishe mgongo wake wenye matatizo na hata wamemzuia asifanye mazoezi yeyote.