Pulis ajiondoa Crystal Palace

Image caption Tony Pulis ajiondoa Crystal Palace ya England

Kocha wa Crystal Palace ya England Tony Pulis amejiondoa katika timu hiyo.

Amefanya hivyo baada ya makubaliano maalum na uongozi wa timu hiyo jana usiku.

Kocha huyo wa zamani wa Stoke City katika siku za karibuni amekaririwa akionyesha kukerwa na uongozi wa timu hiyo kushindwa kusajili wachezaji aliowapendekeza katika msimu huu wa majira ya kiangazi.

Kocha msaidizi wa timu hiyo Keith Millen atabeba jukumu la kuiongoza Palace kwa muda tu na akianza na kibarua pevu kesho huko Emerates mjini London kukipiga na Arsenal.