Arsenal yailaza Crystal palace 2-1

Haki miliki ya picha PA
Image caption Arsenal 2-1 Crystal Palace

Aaron Ramsey alifungia Arsenal bao la dakika ya mwisho ya kipindi cha pili na kuisaidia kufungua kampeini yao ya ligi kuu ya Uingereza kwa ushindi dhidi ya Crystal Palace .

Palace ambao hawana mkufunzi walionesha niya mapema katika kipindi cha kwanza walipofunga kupitia kwa Brede Hangeland

alifuma mkwaju wa kichwa kimiani kunako dakika ya 35 .

Nipe nikupe kati ya timu zote hazikuzaa matunda na Gunners wakienda mapumzikoni wakiwa bao moja nyuma.

Lakini ganga ganga ya mkufunzi Arsene Wenger ilizaa matunda punde baada ya kipindi cha kwanza Laurent Koscielny alipofunga kwa kichwa mkwaju wa Freekick uliopigwa wa Alexis Sanchez katika dakika ya kwanza ya kipindi cha pili.

Mashambulizi ya Arsenal yaliendelea kwa asilimia kubwa ya mechi hiyo lakini kipa Julian Speroni alifanya kazi ya ziada kuwadhibiti vijana wa Wenger.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Arsenal 2-1 Crystal Palace

Bahati yao (Crystal Palace) iliishia dakika ya 89 Jason Puncheon alipofushwa uwanjani baada ya kuoneshwa kadi ya pili ya njano .

Dakika moja baadaye Aaron aliimhakikishia Wenger alama zote tatu kwa bao hilo la Ushindi.

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger alifurahia matokeo akisema kuwa ni motisha kwa vijana wake kujifua kwa mechi dhidi ya mahasimu wao katika mchujo wa kombe la mabingwa barani Ulaya Besiktas .

Katika matokeo mengine ya mechi za siku ya ufunguzi ,Matokeo ya ligi kuu ya EPL:Man Utd iliambulia kichapo cha 1 - 2 dhidi ya Swansea Leicester ikatoka sare ya 2 - 2 na Everton .

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption West Ham 0 - 1 Tottenham

QPR kwa upande wake iliambulia kichapo cha 0 - 1 dhidi ya Hull, Stoke nayo ikipoteza kwa matokeo sawa na hayo dhidi ya Aston Villa. Awali West Brom ilitoka sare ya 2 - 2 na Sunderland ,nayo West Ham ikalimwa 0 - 1 na Tottenham.