Ebola:Ivory Coast kususia mechi

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Ivory Coast kususia mechi na Sierra Leone ikihofia kuenea kwa Ebola

Shirikisho la soka la Ivory Coast limesema kuwa huenda likasusia mechi ya kufuzu kwa dimba la mabingwa barani Afrika dhidi ya wapinzani wao Sierra Leone ikihofia kuenea kwa Ebola.

Mchuano huo ambao umeratibiwa kuchezwa mjini Abidjan tarehe 6 Septemba umeibua taharuki miongoni mwa maafisa wa Afya na serikali kuu inatishia kuipiga marufuku.

Hofu hiyo inatokana na kuenea kwa homa ya Ebola katikamataifa 5 kanda ya Afrika Magharibi ikiwemo Sierra.

Image caption Ivory Coast kususia mechi na Sierra Leone ikihofia kuenea kwa Ebola

"Kwa mujibu wa msemaji wa shirikisho la soka la Ivory Coast Malick Tohe, ikiwa wataruhusiwa kuihamisha mechi hiyo hadi taifa la tatu iwapo CAF itaruhusu.

Tayari Sierra Leone imetaja kikosi cha wachezaji wanaocheza nje ya Sierra Leone ilikuepusha hatari ya kueneza Ebola Ivory Coast .

Sierra Leone imeagiza maafisa wote wa ukufunzi kufanyiwa uchunguzi wa kutosha kabla ya kuingia Ivory Coast .

Image caption Ivory Coast kususia mechi na Sierra Leone ikihofia kuenea kwa Ebola

Shirikisho la soka barani Afrika limekataa katakata kubadilisha kutakapoandaliwa mechi za kufuzu licha ya hatari ya maambukizi .

Hadi kufikia sasa haijulikani iwapo CAF itaichukulia hatua zaidi Ivory Coast iwapo itasusia kuchuana na Sierra Leone au itaruhusiwa kuendelea na mechi za kufuzu.