Liverpool yaifunga Tottenham

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wachezaji wa Liverpool wakisherehekea ushindi

Kocha wa timu ya Liverpool Brendan Rogers amepata furaha nyingine baada ya timu yake kuifunga Tottenham Hotspur kwa mabao 3-0.

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa White Hart Lane, mchezaji mpya wa timu hiyo Mario Balotelli, ameshindwa kuonesha cheche zake katika mechi ambayo ilikuwa ya kwanza kwake tokea ajiunge na timu hiyo baada ya kupoteza nafasi kadhaa za wazi. Goli la penalti la kiungo Steven Gerrad na mawili kutoka kwa Alberto Moreno yalitosha kuizamisha timu ya Spurs katika mchezo huo.

Liverpool walimpoteza mchezaji wao mwenye uwezo wa hali ya juu wa kupachika mabao Luis Suarrez ambaye ametimkia huko Hispania katika club ya Barcelona.

Katika msimu uliopita Suarrez aliifunga Spurs katika michezo yote miwili waliokutana.

Rodgers anaendelea kuwaunganisha wachezaji wake aliowasajili katika msimu wa kiangazi na kuweza kuibuka kidedea katika mchezo wake wa ufunguzi dhidi ya Southarmpton kabla ya kuambulia kipigo kutoka kwa mabingwa watetezi Manchester City jumatatu iliyopita.