Man U yapiku vilabu kumnunua Falcao

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Falcao amenunuliwa kwa kima cha pauni milioni 6

Leo ni siku ya mwisho ya kusajili wachezaji wapya katika vilabu vya soka nchini Uingereza.

Klabu ya Manchester United ndio inalenga kuweka kufuli kwenye dirisha la usajili wa wachezaji msimu huu kwa kumnunua mchezaji mkali wa soka Radamel Falcao.

Man United imempata mchezaji huyo kwa kipindi kizima cha msimu huu kwa mkopo.

Falcao ambaye lazima apitie ukaguzi wa kimatibabu alihusishwa na mpango wa kuihama klabu ya Monaco ambako alisajiliwa kwa kima cha dola milioni hamsini mwaka 2013.

Baadhi waliona taarifa hizo kama fununu tu.

Bila shaka usajili wa Falcao katika Manchester United unaonekana kama mapinduzi kwani vilabu vingi vilikuwa vimemuotea Falcao ambaye anachezea klabu ya Ufaransa ya Monaco.

Falcao ameingiza mabao 11 na kucheza katika mechi 20 za Monaco. Mkataba huo unaipa fursa Manchester United kumnunua mchezaji huyo kwa pauni milioni 43.5 mwishoni wa kipindi cha mkopo.

Klabu ya Louis van Gaal ambayo kama vilabu vingine Ulaya vilifajhamu tu kumhusu mchezaji huyo na uwezo wa kununua katika dakika za mwisho mwisho.

Wakati huohuo, Manchester United itaikopesha Real Madrid mchezaji wake nyota Javier Hernandez.