Kemikali za Xenon na Argon marufuku

Haki miliki ya picha ThinkStock
Image caption Dawa za kuongeza nguvu za Xenon na Argon zapigwa marufuku

Taasisi ya kuzuia dawa za kuongeza nguvu michezoni imezuia Xenon na Argon.

Matumizi ya kemikali hizo mbili, zimepigwa marufuku michezoni.

Ingawa hakujakuwa na vipimo vya wazi vya kuthibitisha athari za kemikali hizo.

Hatua hii inakuja kutokana na kuaminika kuwa wanamichezo walikuwa wakivuta kemikali hizi ili kusisimua seli nyekundu za kuongeza stamina kabla na wakati wa mashindano.