Blatter kuwania muhula wa 5

Haki miliki ya picha AP
Image caption Sepp Blatter atakuwa anawania urais wa FIFA kwa muhula wa tano

Rais wa shirikisho la soka duniani Sepp Blatter, anasema kuwa atawania urais wa shirikisho hilo mwaka ujao.

Utakuwa muhula wake wa tano mamlakani ikiwa atachaguliwa.

Bwana Blatter, ambaye ana umri wa miaka 78, alichaguliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1998.

Amesema kuwa atatangaza azma yake rasmi katika mkutano wa kamati ya shirikisho hilo badaye mwezi huu.

Kiongozi huyo mwenye utata awali alisema kuwa hatagombea muhula mwingine lakini msimako huo umebadilika.