Schumacher atoka hospitali

Haki miliki ya picha AP
Image caption Michael Schumacher

Bingwa wa zamani wa Formula One Michael Schumacher ameruhusiwa kutoka hospitali

Katika taarifa aliyoitoa, Meneja wa bingwa huyo wa zamani wa michezo ya Langa langa, Sabine Kehm amesema mteja wake huyo ataendelea kupata matibabu nyumbani.

Amesema anaendelea vizuri lakini bado kunahitajika muda zaidi kuweza kupona kabisa.

Schumacher alipoteza fahamu baada ya kupata majeraha kichwa kufuatia ajali aliyoipata Desemba mwaka jana nchini Ufaransa alipokuwa akiteleza kwenye barafu.

Schumacher alilazwa kwa muda wa miezi sita katika hospitali moja nchini Ufaransa kabla ya kuhamishiwa katika hospitali ya Lausanne nchini Uswisi mwezi Juni mwaka huu.