Mlinzi Serge Aurier wa I.Coast yuko sawa

Image caption Serge Aurier alipata jeraha baya kiasi cha kuzimia

Mlinzi matata wa Ivory Coast amesema kuwa sawa na madaktari baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.

Madaktari walitoa uamuzi wao baada ya Serge Aurier kujeruhiwa na kuzimia kwa muda wakati wa michuano ya kufuzu kwa kombe la taifa bingwa Afrika dhidi ya Cameroon Jumatano.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, alijeruhiwa baada ya kugongana na kinara wa Cameroon, Stephane Mbia mapema wakati wa kipindi cha pili cha mechi kati ya timu zao.

Ivory Coast ilishindwa na Cameroon kwa mabao 4-1.

Aliondolewa uwanjani kwa kitanda na alionekana kujeruhiwa vibaya.

Lakini Aurier alipata fahamu na kusalia uwanjani kutizama mechi ilipokuwa ikiendelea.

"Alipokea matibabu akiwa katika uwanja wa Ahmadou Ahidjo mjini Yaounde, na msaada huo ndio ulimsaidia kupata fahamu kabla ya kurejea sehemu walipokuwa wachezaji wa akiba. ''