Mechi za kufuzu fainali za kombe Afrika

Mechi za kutafuta tiketi za fainali za kombe la mataifa ya Afrika mwakani huko Moroko ikiwa ni hatua ya makundi ambapo Uganda imeutumia vema uwanja wa nyumbani wa Nelson Mandela kwa kuinyoa Guinea mabao 2 kwa 0

Sudan ikicheza ugenini mjini Pwe Nwah imeambulia kipigo cha magoli mawili bila majibu kutoka kwa Jamhuri ya Kongo.

Bafana Bafana ya Afrika kusini imebanwa nyumbani na mabingwa watetezi Nigeria kwa kushindwa kufungana wakati Malawi imeinyuka Ethiopia 3-2 mjini Blantyre.

Kwenye kundi C Angola wakashindwa kutamba nyumbani kwa kichapo cha mabao matatu kwa 0 kutoka kwa Burkina Faso huku Lesotho ikitoka sare ya bao moja moja na Gabon

Sierra Leone ikawahuzunisha watu wake kwa kuiacha Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ichukue pointi zote tatu kwa ushindi wa mabao 2 kwa 0, kama ilivyokuwa kwa Togo iliyokubali kipigo cha mabao matatu kwa mawili kutoka kwa Ghana.

Mjini Praia…Cape Verde imeirarua Zambia 2 bila, Tunisia wakaitandika Misri 1 bila, nayo Msumbiji ikatoka sare ya 1- 1 na Niger