Kocha Appiah kuaga Black Stars

Image caption Kocha Appiah amesemekana kutofanya vyema hasa wakati w akombe la dunia Brazil

Kocha wa timu ya taifa ya Ghana Kwesi Appiah, ameacha kazi kama kocha wa timu ya taifa baada ya kukubaliana na shirikisho hilo.

Kocha wa zamani Milovan Rajevac, anaonekana na wengi kama mrithi wa kocha Appiah ambaye ameshikilia wadhifa wake kati ya mwaka 2008-2010.

Rajevac, alikuwa ameorodheshwa kama mshauri wa kikosi cha taifa akishirikiana na Appiah.

Shirikisho la soka la Ghana linasema kuwa litatangaza nafasi ya Appiah kabla ya mwishoni mwa Oktoba ambapo Ghana itacheza mechi ya kufuzu dhidi ya Guinea.

'Makosa ya Appiah'

Kosa la kwanza la Appiah ni kukosa kufikisha timu ya taifa katika robo ya fainali za kombe la dunia la mwaka 2014, nchini Brazil na ilikuwa mara ya kwanza kwa Ghana kukosa kufika katika robo fainali.

Wakati alipokuwa uongozini, Rajevac aliongoza Ghana kufika fainali za kombe la taifa bingwa Afrika mwaka 2010 na robo fainali za kombe la dunia miezi michache baadaye.

Appiah amekuwa akishinikizwa tangu kampeni ya Ghana kwenda katika kombe la dunia kuanza ,ambako hawkaufika mbali.

Baada ya timu hiyo kwenda sare na Uganda katika mechi yao ya ufunguzi kutaka kufuzu kwa michunao ya kombe la taifa bingwa Afrika mwaka 2015, wito ulianza kutolewa kuwa Appiah aondoke.

Appiah atakutana na maafisa wa GFA wiki ijayo kujadili swala la malipo yake.