Al Ahly yailaza Zamalek

Image caption Al Ahly iliilaza Zamalek na kutwaa Super Cup

Al Ahly iliilaza mahasimu wao wa jadi Zamalek na kutwaa tuzo la Super Cup ambalo ndilo la kutangulia mwanzo wa ligi mpya ya Misri.

Al Ahly ilikuwa imeweka niya mapema kupitia kwa Walid Soliman aliyegonga mwamba lakini kuanzia hapo mambo yalikuwa suluhu bin suluhu hata baada ya dakika ya 90 ya kipindi cha kwanzo.

Mabingwa watetezi Ahly walitawazwa mabingwa baada ya nahodha wa Zamalek Ibrahim Salah kugonga mwamba.

Ligi kuu ya Misri inaanza baadaye leo huku mashabiki wa timu hizo hasimu wakikatazwa kushuhudia mechi zao.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Mashabiki wa kandanda nchini Misri

Kinyume na ilivyokuwa mwaka uliopita ambapo ligi iligawanya kwa makundi mawili kisha washindi wa kila kundi wakiratibiwa kutoana kijasho na washindi wa pili katika katua ya maondoano mwaka huu hilo limebadilishwa na sasa kila timu itachuana na zingine katika mfumo sawa na ule wa Uingereza.

Asili mia kubwa ya mechi za ligi kuu ya Misri zinachezwa bila ya mashabiki uwanjani baada ya vifo vya mashabiki 70 katika mkasa wa kukanyagana uliotokea mjini Port said mwaka wqa 2012 .