Liverpool yarejea katika ligi kuu Ulaya

Haki miliki ya picha All Sport
Image caption Liverpool yarejea katika ligi kuu Ulaya

Baada ya miaka mitano bila kucheza ligi ya mabingwa wa Ulaya Liverpool leo wanawakaribisha timu ya Lugorets ya Razgrad, Bulgaria kwenye uwanja wao wa Anflid.

Maneja wa Liverpool Brendan Rodgers ana sema nia yako kubwa ni kushinda mashindano haya kwa mara ya sita.

Timu ya Ludogorest ya Bulgaria ni ya pili kutoka Bulgaria kufikia hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa wa Ulaya baada ya Levski Sofia.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Real Madrid itakabiliana na FC Basel

Timu nyingine ya England Arsenal wapo ugenini dhidi ya Borussia Dortmand ya Ujerumani.

Arsenal haitakua na walinzi wake, Mathieu Debuchy na Nacho Monreal, ambao wameumia.

Maneja wa Borussia Dortmand Jurgen Klopp amesema hana uhakika kama mchezaji wake wa kiungo Shinji Kagawa atacheza mechi ya leo.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Arsenal kukabiliana na Dortmund

Mechi nyingine zitakazochezwa leo mabingwa ni watetezi Real Madrid dhidi ya Fc Basel.

James Rodriguez, mshindi wa kiatu cha dhahabu katika kombe la dunia mwaka huu amesema kuwa anaendelea kuyazoea maisha ndani ya Hispania baada ya kujiunga na timu hiyo akitokea klabu ya Monaco, Ufaransa kwa kitita cha paundi 71 milioni.

Mechi zingine za ligi ya mabingwa wa Ulaya zitaendelea hapo kesho.