Marekani bingwa duniani kwa vikapu

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Marekani na Serbia wakichuana

Marekani imetawazwa Mabingwa wa kombe la Dunia wa mchezo wa mpira wa kikapu kwa kuichapa Serbia vikapu 129 kwa 92. Marekani wameutetea ubingwa wao waliouchukua huko uturuki mwaka 2010.

Angola na Senegal ziliiwakilisha afrika ingawa hazikufika mbali sana.

Kombe la Dunia la Mpira wa Kikapu la Mwaka huu wa 2014 lilikuwa toleo la 17 la FIBA Basketball World Cup kwa kuwa hapo awali michuano hi ilifahamika kama FIBA World Championship. Michuaono hii iliyofanyika Hispania ni ya mwishopkufanyika katika mzunguko wa miaka mnne kwani michuano ijayo itafanyika miaka mitano ijayo yaani mwaka 2019 ili kurekebisha hesabu za miaka kuingilia ratiba ya Kombe la Dunia na Fifa.

Katika ligi kuu ya England, ushindi wa Manchester United wa mabao 4-0 dhidi ya Queens Park Rangers umempa nguvu meneja wa timu hiyo Luis Van Gaal na kusema kuwa matarajio yake ni kurejesha taji la ligi katika uwanja wao.

Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya mchezo kuisha amesema, "Nataka kushinda taji la ligi kuu, kama si mwaka huu basi msimu ujao na kama sio ujao basi utakaofuata, nataka kuwapa ushindi mashabiki". Van Gaal, akipata nguvu za ushindi.

Hii leo, Hull City wanawaalika West Ham United katika KC Stadium ama Kingston Communications.

Kwa bahati mbaya Hull City italazimika kucheza bila mshambuliaji bwana mdogo aliyezaliwa mwaka 1990 Abel Mathías Hernández Platero.

Mshambuliaji huyo kutoka Uruguay ni mmoja wa wale waliosajiliwa katika ile tunayoweza kuiita dakika ya tisini akitokea Palermo lakini mashabiki wa Hull watalazimika kusubiri baada ya meneja Steve Bruce kutangaza kuwa kibali cha kufanya kazi hakijapatikana bado. Pengine atatokea katika mfumo wa kuwashangaza mashabiki. Uzuri ni kuwa Muuruguay mwingine Gastón Ezequiel Ramírez Pereyra atakuwepo katika safu.