Kibarua kinachoikabili Liverpool

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Gerrad ''tunakibarua kigumu kuinua viwango vyetu''

Nahodha wa Liverpool Steven Gerrard amekiri kuwa timu hiyo inakazi ya ziada kufanya ilikupunguza pengo la uwezo wao na timu za bara Ulaya ilikushamiri barani huko.

Nahodha huyo aliyasema hayo baada ya kufunga bao la ushindi katika mechi yao ya kwanza ya ligi ya mabingwa barani ulaya tangu mwaka wa 2009.

Liverpool iliilaza Ludogorets 2-1. Mabingwa hao wa mwaka wa 2005 walikuwa wametikisa wavu wakwanza kupitia kwa Mario Balotelli katika muda wa majeruhi ya kipindi cha pili kabla ya furaha yao kukatizwa mara moja na mkwaju wa Dani Abalo.

Hata hivyo nahodha huyo alikabidhiwa jukumu la kuipelekea mbele timu yake kupitia kwa mkwaju wa Penalti mwisho wa mechi hiyo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Gerrad ''ilikuwa bayana hata ushindi huo haukuwa na nguvu kama kawaida yetu''

''tulicheza na tukashinda lakini hivyo sivyo nilivyo tarajia mimi ''

''Najua lazima tufanye kazi ya ziada''

Liverpool, sasa wanajukumu la kuizima FC Basel katika mechi yao ijayo ilikuihakikishia nafasi nzuri ya kusonga mbele katika mkondo wa pili.

Basel jana ilikiona chamtema kuni ilipoambulia kichapo cha mabao 5-1 mikononi mwa mabingwa watetezi Real Madrid.

Kocha Brendan Rodgers alikiri kuwa ni wazi wanakazi ya ziada kufanya ilikuhakikisha watafuzu kwa mkondo wa pili.