Guardiola asema Man U hawana hela

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Guardiola :Manchester United hawana pesa !

Kocha mkuu wa Bayern Munich Pep Guardiola amezua majibizano makali baada ya kudai kuwa Manchester United hawana pesa za kutosha kuwashawishi wachezaji wake kutoka Allianz Arena.

Man chester united imetumia takriban pauni milioni 150 kuwanunua wachezaji akiwemo mchezaji aliyeghari9mu kitita kikubwa zaidi nchini Uingereza Angel Di Maria kutoka Real Madrid.

Maria aliigharimu United takriban pauni milioni 59.7 alipotua Old Trafford.

Sasa Guardiola akizungumza na wanahabari alisema kuwa hana hofu ya kuwapoteza wachezaji wake kwenda Old Trafford. "hawana pesa .

'Samahani hawana hela hawa,'' kocha huyo alinukuliwa akisema .

Image caption Pep:Manchester United hawawezi kuwanunua wachezaji wa Bayern Munich

Guardiola, alikuwa akizungumza kabla ya mabingwa hao wa Bundesliga kuchuana dhidi ya mabingwa wa Uingereza Manchester City .

''Niliwaona wakitumia pesa nyingi tu lakini unajua hawa wachezaji wnyewe wameamua kusalia hapa tu ''

Guardiola, aliwahi hudumu chini ya Louis van Gaal' alipokuwa Barcelona kabla ya wawili hao kutengana Pep alipoondoka kuchukua wadhfa wake mpya kama kocha.