Li Na astaafu tenisi

Li Na  astaafu tenisi
Maelezo ya picha,

Li Na astaafu tenisi

Mchezaji wa kwanza wa Uchina kuwahi kushinda mashindano ya tenisi Grand Slam, Li Na, amestaafu.

Li, ambaye sasa ana umri wa miaka 32, alisema kuwa anaondoka katika mashindano ya tenisi kwa sababu ya majeraha ya muda mrefu, hasa kwenye magoti yake.

Alishinda Grand Slams mara mbili - Frenc Open mwaka 2011 na Australian Open mwaka huu.

Chama cha Tenisi nchini Uchina kimepongeza juhudi zake za kuimarisha mchezo huo nchini mwake.

Hata hivyo waandishi wa habari wanasema kuwa chama cha tenisi cha Uchina hakikubaliana naye mara kwa mara jinsi alivyoendesha mambo yake ya tenisi.