Arsenal yaibamiza Aston Villa 3 - 0

Danny Welbeck akifunga goli dhidi ya Aston Villa
Maelezo ya picha,

Danny Welbeck akifunga goli dhidi ya Aston Villa

Arsenal jumapili wameisambaratisha Aston Villa kwa jumla ya magoli 3 - 0 katika mechi ya Ligi Kuu ya England.

Magoli ya Arsenal yalipatika kwa haraka haraka katika dakika ya 32, 34 na 36.

Mesut Ozil ndiye aliyefungua karamu ya magoli ya Arsenal dakika 32 ambapo baadae Danny Welbeck akafunga goli lake la kwanza akiwa Arsenal katika dakika ya 34 kabla ya Aly Cissokho wa Aston Villa kujifunga katika dakika 36 wakati akijaribu kuuokoa mpira langoni kwake.

Mechi nyingine zilizochezwa siku ya jumapili ilikuwa ni kati ya Queen Park Rangers wakiwa nyumbani ambayo ilitoka sare ya 2 - 2 na Stoke City.

Mame Biram Diouf ndiye aliyekuwa wa kwanza kuandika goli kwa upande Stoke katika dakika ya 11 ambapo baadae katika dakika ya 42 Steven Caulker aliisawazishia QPR goli.

Peter Crouch aliongeza bao kwa upande Stoke katika 41 muda mfupi kabla ya mapumziko japo goli hilo halikudumu kwani katika dakika ya 88 Niko Kranjcar aliisawazishia QPR.

Matokeo mengine ya mechi ya Jumapili ni kama ifuatavyo

  • QPR 2 - 2 Stoke City
  • Aston Villa 0 - 3 Arsenal
  • Burnley 0 - 0 Sunderland
  • Newcastle 2 - 2 Hull City
  • Swansea 0 - 1 Southampton