Jeraha lamtia dosari Azarenka

Maswali yamekua yakiulizwa kama Azarenka ana nafasi ya kufanya vizuri tena
Maelezo ya picha,

Maswali yamekua yakiulizwa kama Azarenka ana nafasi ya kufanya vizuri tena

Katika mchezo wa tenesi mchezaji Victoria Azarenka raia wa Belarus atakosa sehemu iliyobaki ya msimu wa mchezo huo kutokana na jeraha la mguu ambalo limeharibu mwaka wake Mchezaji huyo ambaaye ni mshindi mara mbili katika mashindano ya Australian Open amekwisha kosa miezi mitano katika mwaka huu pekee na kuporomoka kutoka nafasi ya pili mpaka ya 25 katika viwango vya dunia vya mchezo huo.

Azarenka mwenye umri wa miaka 25, alifika robo fainali ya US open mwanzoni mwa mwezi huu na alipangwa kurejea uwanjani katika mashindano ya Wuhan Open huko China.