Chelsea,Man City zatoshana nguvu

Kocha wa Chelsea, Jose Morinho
Maelezo ya picha,

Kocha wa Chelsea, Jose Morinho

Kocha wa Chelsea Jose Morinho amesema timu yake haikutumia vema pengo la mchezaji mmoja wa Manchester city aliyetolewa kwa kadi nyekundu kwakuwa mchezo huo uliomalizika kwa sare ya bao moja kwa moja ulikuwa mgumu na wenye hisia kali.

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye dimba la Etihad siku ya jumapili, mchezaji wa zamani wa Chelsea Frank Lampard ndiye aliyeiokoa Man City kutoka kwenye hatari ya kuziacha pointi zote tatu kwa Chelsea huku vijana hao wa Manuel Pelegrin wakimaliza mchezo huo wakiwa pungufu baada ya Pablo Zabaleta kutolewa kwa kadi nyekundu katika dakika ya 66.

Wakati hayo yakijiri Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini, amebeza mbinu za mpinzani wake Mourinho katika mchezo huo kwa kusema kuwa Vijana wake wa darajani walicheza kama timu ndogo na kukosoa mtindo wao maarufu wa kupaki basi…