Ghana kukosa kocha dhidi ya Guinea

Ghana itachuana na Guinea bila ya kocha mkuu
Maelezo ya picha,

Ghana itachuana na Guinea bila ya kocha mkuu

Ghana haitakuwa na mkufunzi wa taifa timu ya Black Stars itakapokwaruzana na Guinea katika mechi ya kuwania kufuzu kwa kombe la mabingwa barani Afrika mwakani.

Hii ni baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo katika kombe la dunia huko Brazil Kwesi Appiah kuondoka .

Mmoja wa maafisa wakuu wa shirikisho la soka la Ghana Fred Pappoe amesema kuwa Black stars itakuwa kaimu kocha katika mechi hizo mbili za Guinea.

''Nina hakika kuwa lengo letu si kumpata kocha atakayechukua usukani kwa haraka kwa hivyo hatutakuwa tunaskumwa kumpata kocha mpya kabla ya mechi hizo dhidi ya Guinea ''.

''Katika kipindi cha sasa tutakuwa na kaimu kocha tu''

The Black Stars imeratibiwa kuchuana dhidi ya Guinea tarehe 10 Octobahuko Morocco, kabla ya kuwaalika huko Accra siku tano baadaye.

Maelezo ya picha,

Aliyekuwa kocha wa timu hiyop ndiye anayepigiwa upatu kuchukua usukani

Syli Nationale wamelazimika kuandaa mechi yao dhidi ya Black stars ugenini kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini mwao.

Aliyekuwa kocha wa timu hiyo Milovan Rajevac amepigiwa upatu kurejea tena Accra kwa muhula wa pili.

Ghana ilifungua kampeini yake kwa kutoka sare ya 1-1 na Uganda katika mechi yake ya kwanza ya kufuzu kwa dimba la mataifa bingwa Afrika mwakani kabla ya kuilaza Togo 3-2 siku nne baadaye.