Liverpool haina mashaka na Gerrard

Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers
Maelezo ya picha,

Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers

Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers amesisitiza kuwa hana mashaka na Steven Gerrard baada ya kupoteza michezo mitatu kati ya mitano.

Kapteni wa timu hiyo alihaha huku na kule kubadilisha upepo wa mchezo baada ya kutandikwa mabao matatu kwa moja siku ya jumamosi katika michuano ya ligi kuu ya England.

Rodgers amemsifu Gerrard kuwa ni mchezaji mzuri isipokuwa timu tu kwa ujumla haikufanya vizuri, Rodgers anaamini Gerrard bado ana mchango mkubwa katika timu hiyo.