Je Man U ina uhaba wa walinzi?

Haki miliki ya picha PA
Image caption Kocha wa Manchester United Louis Van Gaal

Kocha wa machester United, Louis van Gaal amesema Manchester united ina mlinzi wa kati mmoja tu mwenye uzoefu wakati huu kikosi hicho kinapotarajia kuzipiga na West Ham katika michuano ya ligi kuu ya England.

Marcos Rojo yuko fiti, lakini timu hiyo ina majeruhi kama Chris Smalling ana jeraha la mguu, Phil Jones ana jeraha kwenye, Jonny Evans ana jeraha la kifundo cha mguu na Tyler Blackett hatacheza mchezo huo.

Van Gaal analazimika sasa kuchukua wachezaji kwenye kikosi cha vijana ili kuziba mapengo yaliyopo kwenye timu yake.miongoni mwao ni vijana Tom Thorpe na Paddy MacNair ambao wataungana na kikosi cha kwanza cha Manchester United kwa mara ya kwanza.