Suarez angojewa kwa hamu Barcelona

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Luis Suarez

Luis Suarez anangoja kwa hamu kurejea tena kuichezea timu yake ya Barcelona baada ya adhabu yake ikikaribia kumalizika.

Suarez amecheza mchezo maalum wa kirafiki na timu ya pili ya Barcelona dhidi ya timu ya umri wa chini ya miaka 19 ya Indonesia ambapo Barcelona B imeichapa Indonesia kwa mabao 6 bila.

Kocha wa Barcelona Luis Enrique amesema alitaka Suarez kucheza mechi hiyo ili kuwa katika hamasa ya kimchezo.

Suarez anaruhusiwa kushiriki michezo ya kirafiki pekee , hatashiriki michuano ya la liga mpaka tarehe 24 mwezi oktoba ambapo Barcelona itakutana na Real Madrid