CAF yaondoa marufuku ya Gambia

Image caption CAF yaondoa marufuku ya Gambia

Shirikisho la soka barani Afrika (Caf) limeondoa marufuku ya miaka miwili iliyokuwa imeiwekea The Gambia.

Kauli hiyo inafuatia uchaguzi uliofanyika mwishoni mwa wiki na kumchagua aliyekuwa waziri wa michezo Modou Lamin Kabba Bajo kuywa mwenyekiti wake.

Kamati kuu ya CAF iliondoa marufuku hiyo kufuatia kutekelezwa kwa masharti yaliyokuwa yamewekewa shirikisho hilo la Gambia.

CA Filikuwa imeipiga marufuku Gambia kufuatia udanganyifu wa umri w wachezaji wake .

''Lazima visa vya udanganyifu wa umri wa wachezaji vikome kabisa''barua hiyo ya CAF ilisema.

GFF ililazimika kuanza upya baada ya kamati ya dharura ya FIFA kuifutilia mbali uwakilishi wa shirikisho la Gambia GFF ukiongozwa na Mustapha Kebbeh kufuatia kupatikana udanganyifu wa wa umri wa wachezaji.

Kamati ya muda iliyoundwa ndiyo iliyoshughulika na maandalizi ya uchaguzi huo.

Matukio ya hivi punde yatajadiliwa katika mkutano wa kamati kuu ya FIFA huko Zurich.

Kabba Bajo, 50,alitawazwa mshindi baada ya kuzoa kura 28 kati 51 . Mpinzani wake Buba Mbye Bojang alipata kura 23.

Wengine waliochaguliwa ni Abdoulie Jallow, Ebou Faye na Martin Gomez waliochaguliwa kuwa manaibu wa mwenyekiti .

Alhagie Faye, Adama Lowe, Mam Lisa Camara na Sainabou Cham bwalichaguliwa kuwa wanakamati wa GFF.