Stoke waifumua Newcastle 1 - 0

Haki miliki ya picha Press Association
Image caption Wachezaji wa Stoke City Mame Brium Diouf kulia na wenzake

Goli la mapema la Stoke City lililopachikwa na Peter Crouch kwa njia ya kichwa limezidi kumwongezea tumbo joto boss wa Newcastle Alan Pardew.

Katika dakika ya 15 Crouch aliruka juu na kukutana na krosi iliyotumwa na Victor Moses kutokea kushoto ambapo hakufanya ajizi akaukwamisha mpira wavuni.

Kipigo hicho sasa kimeamsha hasira za mashabiki wa Newcastle juu ya meneja wao Pardew.