Arsenal yaua, Liverpool hoi UEFA

Mechi za klabu bingwa barani Ulaya iliendelea usiku wa kuamkia Alhamis wakati timu kadhaa ziliposhuka dimbani.

Vijana wa mzee Wenger, Arsenal, ulikuwa usiku wao baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Galatasaray ya Uturuki, huku mchezaji mpya wa timu hiyo Danny 'Electric' Welbeck akiondoka na mpira baada ya kuzifumania nyavu za wapinzani wao mara tatu, moja likifungwa na Allexis Sanchez.

Katika mchezo huo Arsenal walimaliza pungufu baada ya kipa wao Wojciech Szczeny kutolewa kwa kadi nyekundu katika dakika ya 60 ya mchezo.

Wakati hayo yakijiri vijogoo wa Anfield Liverpool walikuwa ugenini huko Uswis na kujikuta wakiangukia pua baada ya kufungwa bao 1-0 na FC Basel.

Mabingwa watetezi Real Madrid waliendeleza wimbi la ushindi kwa kuisasambua Ludogorets Razgrad ya Bulgaria kwa jumla ya mabao 2-1. Christiano Ronaldo na Kareem Benzema ndio waliopeleka ushindi kwa vijana hao wa Benabeu.

Kwingineko Atletico Madrid waliialika Juventus ya Italia, hadi mwisho wa mchezo Atletico ikaibuka na ushindi wa goli 1-0.

Borusia Dotmund wakaikaanga Anderlecht kwa mabao 3-0. Bayern Liverkusen wakaiangamiza Benfica kwa mabao 3-1, huku Malmo FF ya Sweden wakawaduwaza Olympiakos ya Ugiriki kwa mabao 2-0.