Jules Bianchi apata ajali

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Jules Bianchi

Katika Mashindano ya mbio za magari ya langa langa ya Formula One dereva wa Ufaransa, Jules Bianchi, yuko katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya kuumia vibaya kichwa chake kutokana na ajali ya kugongana na dereva mwingine katika mashindano ya Japan Grand Prix.

Madaktari wa upasuaji wanaendelea kumhudumia dereva huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye alipoteza fahamu wakati alipofikishwa hospitalini hapo. Bianchi alipoteza uelekeo wa gari lake kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha, hata hivyo ajali hiyo iliyosababishwa na mwendo kasi mkubwa. Dereva wa Uingereza Lewis Hamilton alitangazwa mshindi katika mashindano hayo.