Victor Moses nje kwa jeraha lengine

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Victor Moses alicheza mara ya mwisho kimataifa katika kombe la dunia Brazil

Mchezaji wa Nigeria, Victor Moses atakosa mechi ya kufuzu kwa kombe la taifa bingwa Afrika baada ya kupata jereha la paja.

Moses mwenye umri wa miaka 23, alilazimika kuondoka uwanjani wakati wa mechi kati ya Stoke na Sunderland ambapo Sunderland ilishindwa kwa mabo 3-1 Jumamosi.

Kocha wa mda wa Nigeria,Stephen Keshi amemtaka mchezaji wa Dolphins Emem Eduok kuchukua nafasi ya Moses.

Mkuu wa Stoke,Mark Hughes alisema kuwa Moses, atalazimika kufanyiwa uchunguzi wa kimzaidi wa kimatibabu wakati wa likizo ya kimataifa.

Jerehe la hivi karibuni ni pigo kubwa kwa Moses ambaye hajachezea Super Eagles tangu waliposhindwa katika kombe la dunia nchini Brazil.